Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha wa baadae sasa ni Kocha Mpya

Foto KAF U3120342580677yUG 656x492@Corriere Web Sezioni Danielle De Rossi

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Da capitano futuro a nuovo allenatore della Roma. Hivi ndivyo magazeti ya Italia yalivyoripoti habari ya Daniel De Rossi kutangazwa kuwa kocha mpya wa AS Roma.

Nahodha wa baadaye awa kocha mpya wa Roma, ndiyo tafsiri ya Kiswahili ya maneno hayo ya kiitaliana.

De Rossi aliichezea AS Roma kwa miaka 18, kuanzia 2001 hadi 2019. Tangu alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 2001, mashabiki walimtabiria kuja kuwa nahodha wa timu yao baada ya Francesco Totti.

Ndiyo maana wakamuita Capitano Futuro yaani nahodha wa baadaye (Future Captain). Hata hivyo ilimbidi asubiri sana kıtambaa hadi 2017 pale Totti alipostaafu, ndipo utabiri wa mashabiki ukatimia.

Alikipata kitambaa umri ukiwa umeshaenda sana hivyo hakudumu nacho kwa muda mrefu.

Mwaka 2019 akaondoka Roma na kujiunga na Boca Juniors ya Argentina. Akizungumzia kuondoka kwake Roma, De Rossi alisema anaipenda sana klabu hiyo lakini hana nguvu tena za kuipambania hivyo anapisha wengine wenye nguvu za kuisaidia kusonga mbele.Sasa anakuja kuipambania kutokea kwenye benchi la ufundi.

TIMU YA BABA

De Rossi alianzia soka lake kwenye akademi ya Ostia Mare, aliyojiunga nayo mwaka 1997. Akademi hii ndiyo iliyoibua kipaji cha baba yake, Alberto De Rossi, miaka ya 1970.

Wakati Daniel anajiunga na akademi hiyo, baba yake, Alberto, alipata kazi ya kufundisha akademi za AS Roma.

Mwaka 2000 Daniel akamfuata baba yake, kwenye akademi ya AS Roma. Kwa kufanya hivyo, Daniel akawa amepita njia moja na baba yake.

Alberto De Rossi alidumu kama kocha wa akademi ya AS Roma kuanzia 1997 hadi 2022 alipostaafu.

Yaani Daniel alienda AS Roma mwaka 2000 akamkuta baba yake akiwa kocha wa akademi.

Akapandishwa timu kubwa na kumuacha baba yake kwenye akademi. Akacheza timu kubwa hadi 2019 akaondoka na kuamuacha baba yake kama kocha wa akademi.

Akastaafu soka mwaka 2020 baba yake akiwa bado kocha wa akademi ya AS Roma. Akaenda kusomea ukocha na 2022 akaanza kuifundisha timu ya SPAL ya Serie A…hapo ndipo mzee akastaafu.

Na sasa Daniel anaenda AS Roma kurithi mikoba ya Jose Mourinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live