Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha wa RB Leipzig Willi Orban, achangia Seli kwa mtu asiyejulikana

Willi Orban Mmm Nahodha wa RB Leipzig Willi Orban

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa RB Leipzig Willi Orban anaweza kuukosa mchezo mkali wa timu yake wikendi hii dhidi ya Union Berlin kwa sababu anatarajia kuchangia seli ambazo zitaokoa maisha ya mtu asiyefahamika kwa jina.

Orban, (30) amecheza kila dakika kwa msimu huu na RB Leipzig ya Bundesliga hadi sasa na amekuwa sehemu muhimu ya timu aliyoisaidia kufika nafasi ya 4 ya msimamo chini ya Marco Rose baada ya kumtimua mtangulizi wake Domenico Tedesco mnamo Septemba.

Watamenyana na kikosi hatari cha ligi ya Bundasliga cha Union- Berlin siku ya Jumamosi kwenye dimba la Red Bull Arena lakini beki huyo wa Hungary anaweza kukosekana kwa kuwa hawezi kufanya mazoezi wiki nzima kabla ya mchango wake wa seli.

Upandikizaji wa seli shina huchukua nafasi ya chembechembe za damu zilizoharibika za mtu na kuweka zenye afya kutoka kwa wafadhili na inaweza kutumika kutibu hali zinazoathiri seli za damu, kama vile leukemia na lymphoma.

Hivi karibuni aliarifiwa kuwa alikuwa na mechi, ikimaanisha kuwa kulikuwa na mpokeaji anayefaa wa mchango kutoka kwake na mtu aliye na uhitaji wa aina sawa au sawa na tishu.

Na, kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, Orban anatazamiwa kuchangia seli zake siku ya Jumatano, huku beki huyo akidungwa sindano siku chache zilizopita katika maandalizi ya upasuaji huo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 wa RB Leipzig tangu wakati huo ameelezea furaha yake katika uwezekano wa kuokoa maisha ya mtu.

Alisema kuwa “Bila shaka nilishangaa mwanzoni nilipopata taarifa kwamba ninastahili kuwa mfadhili.

“Lakini sikuwahi kuwa na shaka yoyote, nilitaka kushughulikia mchango huo moja kwa moja. Huu ni uwezekano wa kuokoa maisha ya mwanadamu kwa juhudi kidogo sana, hakuna maoni mawili kwangu.

“Ninatumai sana kwamba mchango wangu unaweza kusaidia kumponya mpokeaji kabisa.’

Mchakato wa kuchukua seli za shina kutoka kwa Orban utafanyika huko Dresden na unatarajiwa kudumu kwa masaa kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live