Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Simba Queens atoa neno kuelekea mchezo ujao

Fatuma Fetty Densa Fatuma Issa ‘Fetty Densa’

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya As FAR Rabat, Nahodha wa Simba Queens, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ amesema wanaenda kupambana kwenye mchezo ujao.

Simba Queens kwa sasa ipo nchini Morroco kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) kwa upande wa wanawake.

Kwenye mchezo huo wa kwanza uliopigwa juzi jumapili ulimalizika kwa Simba Queens kupoteza kwa bao 1-0 hivyo mchezo ujao wanatarajia kukipiga dhidi ya Determine ya nchini Liberia.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Densa alisema “Tulijitahidi kupambana kwa nafasi yetu lakini naamini haikuwa bahati yetu.

“Tulijitoa kwa kila namna kuhakikisha tunapata ushindi lakini nadhani viongozi wa benchi la ufundi waliona wapi tumekosea hivyo watafanya marekebisho.

“Kwenye mchezo ujao tutajitoa na kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ushindi na kuweza kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live