Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Serengeti Boys ajilipua

47832 SB+PIC

Thu, 21 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nahodha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Morice Abraham amesema ana matumaini kikosi hicho kitatwaa Kombe la Afrika katika fainali zitakazofanyika Aprili 14 hadi 28 nchini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Abraham alisema maandalizi mazuri wanayopata na hamasa ya kucheza nyumbani vitaongeza morali ya kutwaa ubingwa ingawa anatarajia upinzani.

“Tupo nyumbani tuna kila sababu ya kuchukua ubingwa tukiwa hapa na hilo ndilo lengo letu kwasababu tunataka kuandika historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

“Tuna morali ya juu na lengo letu ni kuhakikisha Taifa linapata heshima, sisi hatutawaangusha Watanzania, lakini tunawaomba wajitokeze kwa wingi tunapokuwa uwanjani,” alisema nahodha huyo.

Katika hatua nyingine, kocha wa timu hiyo Oscar Mirambo amedokeza kuwa nyota 28 ndio watashiriki kambi ya mwisho ya maandalizi ya timu hiyo kabla ya fainali za Afrika kuanza jijini Dar es Salaam.



Chanzo: mwananchi.co.tz