Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Ruvu Shooting akiri mambo magumu Ligi Kuu

Ruvu Shooting  208 1080x640.png Nahodha Ruvu Shooting akiri mambo magumu Ligi Kuu

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha na Mshambuliaji wa Ruvu Shooting Abrahaman Mussa, amewataka wachezaji wenzake kupambana katika mechi tatu zilizobaki ili wacheze hatua ya mtoano.

Ruvu Shooting inashika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 20 na imebakiza michezo mitatu dhidi ya Simba SC, Singida Big Stars na Dodoma Jiji.

Mussa ambaye kwa sasa yuko nje ya uwanja mwezi mzima baada ya kuumia mguu, amesema wana hali ngumu lakini hawawezi kukataa tamaa hadi ligi imalizike.

“Tuna hali mbaya kwani tuko mwisho katika a msimamo lakini kila na tamaa kwani mara tumekuwa tukikumbushana wenzangu kuendelea kupambana bila kukata tamaa kwani ligi bado inaendelea na lolote linaweza kutokea,”

“Mimi nawaomba wachezaji wenzangu wajitume, kama wakishindwa kutimiza pointi za kubaki moja kwa moja basi wacheze hata hatua ya mtoano ambayo inaweza kutunusuru.” Amesema

Mussa amesema jambo kubwa lililosababisha timu hiyo msimu huu ikawa nafasi ilyopo sasa ni kutokana na wachezaji muhimu kwenda kozi za mara mara za kijeshi hivyo kuiathiri timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: