Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Msumbiji agoma kutundika Daluga

Pelembe Nahodha wa Msumbiji, Elias Domingues 'Pelembe'

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya wengi kufikiri kuwa fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu huko Ivory Coast zingekuwa za mwisho kwa nahodha wa Msumbiji, Elias Domingues 'Pelembe' winga huyo amesema hana mpango wa kustaafu na anatamani kucheza fainali zinazofuata ambazo zitachezwa.

Pelembe aliiongoza Msumbiji katika fainali zinazoendelea ambapo timu yake imeishia katika hatua ya makundi baada ya kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi B nyuma ya Cape Verde, Misri na Ghana huku akiwa na umri wa miaka 40.

Pamoja na umri wake mkubwa wa miaka 40, Pelembe ametamba kuwa suala la kustaafu kuitumikia Msumbiji hivi sasa sio kipaumbele chake na anataka kuendelea kuichezea kwa muda mwingine zeidi.

"Bado nina miguu ya kuiwakilisha timu ya kwetu sote," alisema Pelembe muda mfupi baada ya timu ya taifa ya nchi hiyo kutua Maputo ikitokea Ivory Coast.

Winga huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns, Supersport United na Bidvest Wits za Afrika Kusini ameichezea Msumbiji idadi ya michezo 101 katika mashindano tofauti na kwenye Afcon safari hii, amecheza idadi ya michezo yote mitatu ya timu yake.

Akizungumzia ushiriki wa timu yake kwenye Afcon mwaka huu, Pelembe alisema kuwa amefurahishwa na kiwango bora ambacho timu yake imekionyesha kwenye mashindano hayo ingawa haikufanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora.

Pelembe alisema wachezaji wengi ndio walikuwa wanashiriki fainali za Afcon kwa mara ya kwanza hivyo wamepata uzoefu ambao utawasaidia katika mashindano yaliyo mbele yao.

Chanzo: Mwanaspoti