Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Kagera awachimba mkwara Yanga

Yanga Avic Vs Mamelodi Nahodha Kagera awachimba mkwara Yanga

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache kabla ya mchezo wa Yanga SC dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, nahodha wa Kagera Sugar, Abdallah Mfuko amesema hawaiogopi Yanga SC ila wanaiheshimu.

Nahodha huyo amesema hayo jana na kuongeza kuwa kikosi chao kimejipanga vyema kupata pointi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.

“Huu ni mchezo kama mchezo mwingine ambao timu yetu imecheza. Hatuna sababu ya kuwaogopa Yanga SC maana huu ni mpira na sio ngumi. Hivyo tutawapa heshima, lakini hatuwaogopi,” alisema Mfuko.

Mchezo wa kwanza wa timu hizo uliofanyika katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba ulimalizika kwa matokeo ya sare tasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live