Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nagelsman: Musiala, Bellingham walistahili Tuzo mbele Gavi

Julen Nagelsman Nagelsman: Musiala, Bellingham walistahili Tuzo mbele Gavi

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Fc Bayern Munich Julien Nagelsman kutoka nchini Ujerumani anaamini Tuzo ya kinda bora wa mwaka ambayo amepata kinda wa klabu ya FC Barcelona hakustahili na amesema Jamal Musiala na Jude Bellingham walistahili kubeba tuzo hiyo maarufu kama Kopa Trophy.

Katika tuzo hizo ambazo kinda wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Pablo Gavira alishinda huku Musiala na Bellingham wakishika nafasi ya tatu na ya nne na kiungo wa Real Madrid Mfaransa Eduardo Camavinga akimaliza nafasi ya Pili.

Nagelsman anaamini Musiala na Bellingham walikua na msimu mzuri zaidi ukilinganisha na Gavi ambaye ndo mshindi wa tuzo hiyo kitu ambacho kocha huyo anaona vijana hao wamedhulumiwa lakini hakusita kumpongeza mshindi wa tuzo hiyo.

“Kwa macho yangu Bellingham na Musiala walikua na msimu mzuri zaidi kuliko mshindi. Gavi ni mchezaji mzuri, Ninafurahia pia alichokipata” Alisema kocha huyo

Pia kocha Nagelsman aliulizwa kuhusu mchezaji wake kutokuhudhuria hafla za tuzo hiyo akaeleza mchezaji huyo ana majukumu ya timu katikati ya wiki ambapo watacheza mchezo wao wa DFB Pokal dhidi ya Augsburg.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live