Baada ya siku chache kukamilisha usajili wa golikipa mwenye uraia wa Mali, Diarra Djigui hatimaye klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa golikipa mwingine kutoka klabu ya Aigle Noir ya Burundi.
Mlinda mlango huyo ni Erick Johola ambae amesainiwa na Wanajangwani ikiwa ni sehemu ya kuziba mapengo ya magolikipa walioachwa awali na klabu hiyo Farukh Shikhalo na Metacha Mnata.
Johore mwenye asili ya Tanzania aliekuwa anakipiga katika klabu ya Aigle Noir inayoshiriki Ligi kuu ya Burundi, atakabiliana na changamoto ya kugombea namba kati yake na Diarra Djigui ambae nae amesaini hivi karibuni kwa Wananchi.
Yanga inajiandaa vilivyo ili kuisimamisha Simba SC ambayo imebeba ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo.