Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nafasi mpya ya Tanzania kwenye viwango vya FIFA

5202 TAIFA Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Tanzania yapanda kwa nafasi mbili kwenye orodha ya viwango vya ubora vya soka Duniani vinayotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) sasa inashika nafasi ya 135.

Taifa la Ubeligiji ndilo linaloshika nafasi ya kwanza Duniani kwenye orodha hiyo.

Tanzania imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 137 hadi ya 135, hii ni kwa mujibu wa orodha mpya iliyotolewa leo na FIFA.

Kwenye orodha ya mwisho ya viwango vya ubora ya Mei 27, 2021 Tanzania ilikuwa nafasi ya 137 na jumla ya alama 1088 lakini kwa mujibu wa viwango vilivyoachiwa leo Agosti 12, Tanzania imepanda kwa nafasi mbili na imeongeza alama sita (6) na sasa ina jumla ya alama 1094.

Hii ni kutokana na timu ya taifa Taifa stars kushinda mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Malawi kwa ushindi wa mabao 2-0, mchezo ambao ulichezwa Juni 6, 2021.

Kwa barani Afrika Tanzania ni ya 39 kati ya mataifa 54 ambayo ni wanachama wa FIFA na CAF. Lakini vinara wa ubora barani Afrika ni timu ya taifa ya Senegal ambayo pia ni ya 21 Duniani.

Chanzo: eatv.tv