Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nafasi mbili kaa la moto Championship

Dgsr Nafasi mbili kaa la moto Championship

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati ligi ya Championship ikiendelea leo kwa baadhi ya mechi, vita ya nafasi mbili za juu imeonekana kuwa mtihani kwa timu tatu huku Mbeya Kwanza nao wakiongeza presha kubwa.

Vita hiyo imekuja baada ya Pamba Jiji kuichapa Transit Camp bao 1-0 na kupanda Hadi nafasi ya pili kwa pointi 47, sawa na Ken Gold.

Hata hivyo, Pamba Jiji itakuwa wanaomba dua mbaya kwa wapinzani wao, Biashara United waliopo nafasi ya tatu ambao watakuwa uwanja wao wa nyumbani Karume mjini Musoma leo Februari 15, kuwakaribisha Polisi Tanzania.

Biashara United iliyoshuka daraja msimu uliopita, iwapo itashinda mechi hiyo itapaa kileleni kwa pointi 49, huku ikiiombea Ken Gold ilyodumu muda mrefu kileleni ipoteze mchezo wao dhidi ya Cosmopolitan utakaopigwa leo Alhamisi jijini Dar es Salaam.

Wakati wababe hao wakiombeana dua mbaya, Mbeya Kwanza nayo inazidi kuongeza presha ambapo kama kesho itashinda mchezo wake dhidi ya Mbuni huko mkoani Mtwara, itafikisha pointi 45 ambazo zitawarejesha kwenye mlango za kurudi Ligi Kuu msimu ujao.

Msimamo uko hivi, hadi sasa Ken Gold inaongoza kwa wastani wa mabao ya kufunga ikilingana pointi na Pamba Jiji (47), huku Biashara United ikiwa na pointi 46 na Mbeya Kwanza nafasi ya nne kwa pointi 42.

Kocha Mkuu wa Ken Gold, Jumanne Challe, amesema kwa sasa akili zao zipo kwenye mchezo ujao (leo), dhidi ya Cosmopolitan ambayo ikifanikiwa kushinda itajiweka kwenye njia nzuri ya kuandika historia ya kucheza Ligi Kuu.

"Baada ya mchezo wa leo ugenini, tutarejea nyumbani michezo miwili dhidi ya Biashara United na Pamba Jiji ambapo tukishinda huenda tukatangaza kupanda Ligi Kuu, lakini nguvu zetu kwa sasa tunaiwaza Cosmo, " amesema kocha huyo.

Kocha mkuu wa Mbeya Kwanza, Michael Mnyali amesema hawajapoteza matumaini yao isipokuwa wanaendelea kusuka kikosi chao kiufundi kupata ushindi kwenye mechi zote zilizo mbele yao.

"Tunawaandaa wachezaji kujua umuhimu wa kila mchezo kuanzia wa kesho Ijumaa dhidi ya Mbuni, lakini tukihesabu mechi zote tupate ushindi kisha kuona hatma yetu," amesema Mnyali.

Chanzo: Mwanaspoti