Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nado kuliamsha upya Azam

Iddy Nado Back Nado kuliamsha upya Azam

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Winga wa Azam FC, Iddi Seleman ‘Nado’ baada ya kutoonekana uwanjani kwa zaidi ya miezi nane akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye mechi ya Ligi Kuu Novemba 30,2021 dhidi ya Mtibwa Sugar timu yake ikishinda 1-0, sasa yupo tayari kuanza kukiwasha baada ya kupona.

Akizungumza kocha mkuu wa Azam Abdihimid Moallin alithibitisha utayari wa Nado na kueleza amepona na alikuwa kwenye programu za timu tangu kipindi cha maandalizi ya msimu huu ‘pre season’ iliyofanyika nchini Misri kwenye mji wa El Gouna.

“Yupo fiti, ujue alikaa nje kwa muda mrefu hivyo alihitaji muda wa kutosha kufanya maziozi na kurudi kwenye ubora wake,” alisema Moallin na kuongeza;

“Hatukutaka kumuwahisha kumpa mechi lakini kwa sasa anaweza kucheza na mtamuona kwani tutakuwa tukimpa muda taratibu ili arudishe hali ya kujiamini na kushindana.”

Kipindi chote hicho alichokaa nje Nado alikuwa akiuguza jeraha lake la (Anterior Cruciate Ligament) alilofanyiwa oparesheni na kurejea kwake imekuwa furaha kwa uongozi na mashabiki wa Azam kwani akiwa fiti amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu.

Kwa upande wake Nado amefunguka “Ni muda mrefu nimekaa nje lakini kwa sasa nipo tayari, niwaahidi tu mashabiki zangu kuwa nitaendelea nilipoishia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz