Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nado awatoa hofu mashabiki Azam

Nado Pic Data Nyota wa Azam, Idd Seleman ‘Nado’ (kulia)

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idd Seleman ‘Nado’ alifunga bao lake la kwanza msimu huu, huku chama lake la Azam FC likipasuka mbele ya Polisi Tanzania na sasa amewataka mashabiki wa klabu hiyo wasiogope kwa matokeo iliyopata mpaka sasa akisema ni upepo tu unapita ila raha inakuja kwani msimu huu wapo bora kinoma.

Azam ilichapwa mabao 2-1 mjini Moshi ikiwa ni siku chache baada ya kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union na kuifanya ipate alama moja tu katika mechi mbili za awali za Ligi Kuu Bara msimu huu na Nado alisema wameteleza ugenini kwa kushindwa kutumia nafasi walizopata, ila watu wasiikatie tamaa.

Kiungo mshambuliaji huyo ameliambia Mwanaspoti; “Ni mapema sana kuhukumiwa kwa kupoteza ugenini sisi bado ni bora na uongozi umefanya usajili bora ambao utatoa kajibu muda mchache mbele sasa tunakubaliana na kila linalozungumzwa dhidi yetu.”

“Ubora wetu utaondoa kila kinachozungumzwa sasa tukianza kukusanya pointi, hatuna timu mbovu tutaendelea kuipambania timu iweze kufikia makengo tuliyojipangia mwanzoni mwa msimu,” alisema Nado aliyesajiliwa Azam misimu miwili iliyopita akitokea Mbeya City.

Aliongeza kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri huku akikiri kuwa bado hawajatengeneza kikosi cha kwanza kutokana na ongezeko la nyota wapya hivyo wakikaa sawa watakuwa bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live