Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nacho: Hakuna kama Real Madrid

Nacho Fenandez.jpeg Nacho Fernandez

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: Tanzaniawwb

Beki wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Hispania Nacho Fernandez ameweka wazi hana shaka juu ya mkataba wake ndani ya klabu hiyo na kusema haoni sehemu bora zaidi ya klabu hiyo.

Nacho Fernandez amekua akiitumikia klabu ya Real Madrid na mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, Lakini beki huyo ameonesha hana shaka juu ya kuongezewa kwa mkataba ndani ya klabu hiyo kwani haoni timu nyingine bora ya kwenda zaidi ya wababe hao wa soka nchini Hispania.

Klabu ya Real Madrid imekua na utaratibu wa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja mmoja kwa kila mchezaji wake ambaye amefikisha umri wa miaka 30 na beki huyo ana umri wa miaka 33 kwa sasa, Hivo ni wazi kama ataongezewa mkataba ndani ya timu hiyo utakua mpaka mwezi Juni 2024.

Nacho ameanza kuitumikia timu ya wakubwa ya Real Madrid kuanzia mwaka 2011 hivo mpaka sasa ana miaka takribani 12 ndani ya timu hiyo na uwezekano wa kuongezewa mkataba wa kusalia ndani ya klabu hiyo ni mkubwa kwani amekua mchezaji muhimu kwa kipindi kirefu ndani ya timu hiyo.

Beki Nacho ni mchezaji alietoka kwenye akademi ya Real Madrid na kupandishwa timu ya wakubwa akiongea na waandishi wa habari alionesha pesa sio kipaumbele kwake, Lakini anachotaka ni kupewa umuhimu ndani ya timu hiyo na kumalizia kwa kusema maamuzi atayafanya kwa utulivu na klabu yake.

Chanzo: Tanzaniawwb