Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naby Keita achagua kwenda nyumbani badala ya Uwanjani

Naby Keita Ujerumani Naby Keita

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa klabu ya Werder Bremen, Naby Keita, Juzi hakupanda basi la timu kuelekea uwanjani wakati wanaenda kuikabili klabu ya Bayer Leverkusen.

Keita alielekea nyumbani badala ya uwanjani baada tu ya kocha kumuacha nje ya kikosi hapo jana.Kocha ameweka wazi kuwa ataongea nae pamoja na wakala wake kuyamaliza.

"Tutaongea nae kuhusu hili tukio, pia tutaongea na wakala wake kesho [leo] kuhusu tatizo hili ili tujue tunaendaje mbele."

Hata hivyo Werder Bremen walipoteza kwa jumla ya goli tano [5-0] na Bayer Leverkusen wakatawazwa mabingwa wa Bundesliga baada ya kufikisha alama ambazo hakuna timu nyingine itazifikisha msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live