Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabii Meja; Shabiki maarufu wa Simba ahamia Yanga

Meja WA0004 Nabii Meja; Shabiki maarufu wa Simba ahamia Yanga

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Simba SC ambaye alipata umaarufu baada ya kushirikishwa na Kingwendu kwenye wimbo wa kitambo kidogo uitwao (Mapepe), Nabii Meja ametangaza kuhamia Yanga SC.

Akizungumza live kupitia EA-TV amesema; "Nimehama Simba nimehamia Yanga rasmi, kilichonifanya nihame Simba ni kutafuta furaha. Sioni "Progress" ndani ya Klabu ya Simba, ukiangalia namna timu inavyokwenda huoni kama watu wana nia ya kuipeleka mbali, nikaona napoteza muda tu.

"Jezi nimenunuliwa na washikaji zangu pale Karume baada ya kuonesha nia wakasema basi acha waninunulie jezi. Raha unaweza ukapewa lakini furaha unaitafuta. Yanga kuna furaha na wana progress nzuri tofauti na Simba ambao wanaendesha timu kwa propaganda.

"Mimi nilikuwa Simba kwa kurithi kutoka kwa baba yangu, alitaka watoto wake tuwe Simba ikabidi niwe shabiki wa Simba kwa sababu ya kuogopa kunyimwa ugali. Sijawahi kuwa mwanachama wa Klabu ya Simba, ningekuwa Mwanachama basi wangekuwa wameshanifungia.

"Nimerithi kuishabikia Simba kutoka nyumbani kwa sababu bila kushabikia Simba hauwezi Kula UGALI. Shabiki lazima uhame hame ili kutafuta sehemu ambayo unaweza kupata furaha. Nitapeleka maombi Klabu ya Yanga wakikubali nitakuwa mwanachama wa klabu hiyo.

"Simba nilikuwa shabiki lakini Yanga natamani kuwa Mwanachama kwa sababu ni KLABU NINAYOIPENDA KWA MUDA MREFU. Naomba wanipokee na wanikaribishe kwenye matawi. Niko tayari kuwa Mwanachama wa Yanga SC.

"Sijawahi kutumika kuichafua klabu ya Simba, mimi nimekuwa nikisema madhaifu ya Klabu ya Simba Sijawahi kutumika kuchafua timu au kumsifia tajiri yeyote yule," amesema Nabii Meja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live