Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi yupo sana Yanga, uongozi wamkabidhi timu

Nabi Pc Data Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuteleza sio kuanguka, ndicho kinachotokea ndani ya kikosi cha Yanga kwa sasa baada ya kuanza vibaya katika michuano ya Kimataifa na kila mmoja akijua kocha Mkuu wa Timu hiyo ataondolewa kumbe sivyo ilivyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha, amefunguka kuwa licha ya baadhi ya mapungufu yanayoonekana kwenye kikosi cha timu yao, lakini uongozi wa klabu hiyo una imani kubwa na kocha wao, Nasreddine Nabi, hivyo apewe muda kutengeneza timu bora Afrika.

Licha ya kuanza vizuri msimu huu kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii na kuvuna pointi sita katika michezo miwili ya kwanza ya Ligi Kuu Bara, Yanga imekosolewa kuwa na mapungufu ya kiufundi ikiwemo muunganiko wa timu na utimamu wa mwili.

“Tumefanya usajili wa wachezaji bora msimu huu na tuna malengo ya kufanya mambo makubwa, hasa kwa kuzingatia matarajio ambayo mashabiki wetu wamekuwa nayo kwa kipindi cha misimu minne iliyopita' amesema Senzo.

“Lakini ni jambo lililowazi kuwa hatupaswi kuwa na presha ya matokeo kwa sasa kwa kuwa idadi ya wachezaji wapya ambao tumewasajili tunahitaji kumpa kocha wetu Nabi muda wa kutosha zaidi ili kutengeneza muunganiko wao, naamini tukifanikiwa hapo na kwa maendeleo tunayoyaona siku baada ya siku bila shaka tutakuwa miongoni mwa timu bora Afrika.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live