Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi mipango yote kwa Waarabu

Nabi Pic Xxx Nabi mipango yote kwa Waarabu

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikirejea kutoka Mwanza ilipocheza mechi ya Ligi Kuu na kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, kocha Nasreedine Nabi amesema akili yao sasa ni jinsi gani watashinda mechi yao dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Mkapa, ikiikaribisha Club Africain, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza jana, Nabi alisema anajua mchezo huo utakuwa mgumu, lakini mazoezi yao na maombi yake yatakuwa katika wachezaji wake kucheza vyema kwenye kukaba watakapokuwa wanashambuliwa.

Nabi alisema Yanga inaweza kushinda mechi hizo, lakini ushindi wake utatokana na jinsi itakavyopunguza makosa ya kulinda kuanzia eneo la kiungo kwenda kwa mabeki wake.

“Hii ni mechi ngumu (dhidi ya Club Africain), tunakwenda kukutana na timu ambayo inacheza kwa utamaduni wa Watunisia, kupambana sana kwa nguvu, hii ni lazima tuwe na mabadiliko makubwa katika nidhamu ya ukabaji na kuzuia kwenye eneo letu la ulinzi.

“Najua tunaweza kushinda kwa kuwa tuna ubora wa kutengeneza nafasi na hata kuzitumia, kule mbele tunatakiwa kucheza kwa faida ya timu maombi yangu na nitazungumza sana na wachezaji juu ya umuhimu wa nidhamu ya wakati tumepoteza mpira na wakati tunao,” alisema Nabi.

Yanga ilishuka katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutolewa na Al Hilal kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, uliotokana na sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Mkapa na kipigo cha ugenini (1-0).

Nabi anaonekana kutaka kuchukua tahadhari kutokana na kuwepo kwa makosa mengi katika safu ya ulinzi kwenye michezo ya hivi karibuni.

“Ni kweli tunahitaji kufanya kazi kubwa katika eneo la ulinzi, nafurahi kuona Bacca (Ibrahim) anakuja vizuri kwa kupata nafasi kikosini, atatuongezea kitu zaidi, lakini kwanza ni kufuta makosa na kushambulia zaidi, aliongeza kocha huyo raia wa Tunisia.

Mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele alisema kuekekea mechi hiyo wataingia na akili ya kusaka ushindi huku wakitaka kuhakikisha hawaruhusu bao lolote.

“Tuliumizwa baada ya kutolewa dhidi ya Al Hilal lakini mechi hii tunataka kuwa tofauti, tunataka kutafuta mabao lakini tukikumbuka kwamba ni hatua mbaya kama wapinzani wetu watapata bao lolote,” alisema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live