Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi kufanya kikao kizito na Rais FAR Rabbat

Nabi Far Rabbat Nabi kufanya kikao kizito na Rais FAR Rabbat

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga Nasreddine Nabi amekiri kupokea Ofa kutoka kwenye klabu ya Kaizer Chiefs inayoshiriki Ligi kuu nchini Afrika Kusini.

Kocha huyo ambaye amekosa ubingwa wà Ligi kuu nchini Morocco akiwa na FAR Rabat mbele ya Raja Casablanca amekuwa kwenye rada za Kaizer Chiefs kwa muda mrefu.

Hata hivyo amesema kuwa Kaizer Chiefs sio timu pekee iliyomfuata na kuhitaji saini yake baada ya kuthibitisha kuwa anaondoka FAR Rabat.

"Nimepokea ofa nyingi sana sio tu ya kutoka Afrika Kusini lakini nitakuwa na kikao na Rais wa FAR Rabat Mohamed Haramou kulizungumzia hili."

"Kwa sasa mawazo yangu yapo kwenye nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Maghreb Fez. Najaribu kuongeza ari ya kupambana kwa wachezaji na kuwaambia bado tuna nafasi ya kubeba kombe la 'Throne Cup'."

Nabi bado ana mkataba na Rabat utakaomfanya asalie kikosini hapo hadi June 2025 lakini Chiefs itahitajika kununua mkataba wa kocha huyo wa zamani wa klabu ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live