Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awataka Rivers United

Nasreddine Nabi El Prof Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefunguka kwa njia ya simu kwamba wana timu ambayo inaweza kupambana na yoyote kati ya hizo lakini akasema ungekuwa uwezo wake angeomba wapangwe aidha na Rivers United au USM Alger.

Nabi alisema anawatamani sana Rivers ili aweze kulipa kisasi kwani waliwahi kumwondoa vibaya msimu wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nakumbuka ilikuwa ni mwanzo na tulikuwa na changamoto nyingi nadhani hii nafasi tukikutana nao nitafurahi ili nao wajue ubora wetu halisi wa sasa, ukweli lingekuwa ombi langu ningecheza na hawa,” alisema Nabi

Aidha Nabi aliongeza kama sio Rivers basi atafurahi kuwapokea USM Alger, “Ukikutana na timu za Kaskazini ni jambo zuri kuanzia kwao kisha kumalizia kwetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live