Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awapigia hesabu kali Simba

Kaze Nabi Makocha wa Yanga, Kaze na Nabi

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema anamalizana kwanza na Geita Gold katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kisha inaanza mipango ya pambano lao la Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.

Nabi alisema kushinda pambano lao la Jumatano dhidi ya Azam imewaongezea morali na sasa wanaenda kuvaana na Geita katika mechi ya ASFC ili kuhakikisha kwanza inasonga mbele kisha kutumia siku 20 zilizosalia kujiandaa dhidi ya Simba.

Kocha Nabi alisema anataka kwanza kuhakikisha wanashinda mechi ya robo fainali dhidi ya Geita ili kuwa na uhakika wa kwenda kwenye hatua inayofuata.

Nabi alisema kulingana na ratiba yao ilivyokuwa ushindi wa mchezo dhidi ya Azam umeongeza morali na hali ya ushindani kwa wachezaji wake kuelekea kwenye michezo yao mingine.

Alisema kuna walioamini Yanga itakuwa na wakati mgumu kushinda dhidi ya Azam ila kazi kubwa waliyofanya wachezaji wake kupambana muda wote wa mchezo wameendeleza rekodi yao ya kutokupoteza kwenye ligi hadi wakati huu.

“Kulingana na muda tuliyokuwa nao wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba tutakuwa na programu maalumu ya kufanya mazoezi na kucheza mechi zile za ndani ili kuona namna gani tunafanikiwa na kwenye mapungufu kuboresha kabla ya kukutana nao,” alisema Nabi na kuongeza;

“Kabla ya kucheza na Azam tulipata muda wa kutosha kufanya mazoezi ikiwemo kucheza mechi za kirafiki, tulipata muda wa kutosha kuwafuatilia wapinzani vile wanacheza ubora na mapungufu yao tulienda kutumia na kupata ushindi.”

“Hadi ikifika siku ya mechi naamini kuna baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza waliokuwa majeruhi watakuwa wamerejea na kuongeza ubora wa timu yetu kwenye mechi hiyo kuwa nchini.

“Hakuna mechi ya dabi iliyokuwa rahisi, ushindani mkubwa kwenye mechi utakuwepo ila naimani wachezaji wangu watafanya vizuri na kushinda kwani ikiwa hivyo tutakuwa kwenye eneo zuri la kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi baada ya kushindwa kufanya hivyo misimu minne iliyopita.”

Wakati Yanga ikionekana kuwa na ratiba hiyo upande wa Simba, ratiba inaonekana kuwabana kwani kabla ya mchezo huo itakuwa na mechi nne ngumu katika mashindano matatu tofauti.

Simba itacheza mechi ya kiporo katika ligi dhidi ya Polisi Tanzania kesho Jumapili, baada ya hapo siku tatu mbele itakuwa na kibarua cha robo fainali ya ASFC dhidi ya Pamba Aprili 13.

Baada ya hapo Simba itacheza mechi ya kwanza ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 17, dhidi ya Orlando Pirates kabla ya kwenda kurudiana nao Aprili 24, kule Afrika Kusini.

Kutokana na ratiba hiyo kikosi cha Simba kinaweza kurudi nchini kati ya Aprili 25-26, kisha watakuwa na siku si zaidi ya tatu kufanya maandalizi ya kutosha ili kuwakabili watani zao Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live