Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awaonya nyota wake

5c86de2fd3f1bed405d4ceb1a0ece372 Nabi awaonya nyota wake

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewaonya nyota wake kutosheherekea kupitiliza baada ya kuifunga Yanga na kusahau fainali ya Kombe ya Shirikisho.

Yanga itakutana tena na Simba katika fainali ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa Julai 25 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Katika mchezo wa Ligi Kuu, Yanga iliwafunga watani zao kwa bao 1-0.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam hivi karibuni, Nabi alisema: “Ni kweli tunasherehekea kuifunga Simba, lakini hatutakiwi kusahau kwamba kuna fainali inatusubiri.”

“Ni wazi mechi ijayo ya fainali itakuwa ngumu inabidi tuendelee kujipanga vizuri tukijua wazi karibu wachezaji wote wa Simba ni hatari. “

Alisema Wekundu hao wanaweza kuja kwa hasira ya kutaka kulipiza kisasi hivyo, watakuja kwa nguvu, ni muhimu kwao kujipanga kwa mchezo huo wa kuwania Kombe la FA.

Bingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam huwakilisha taifa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ndiye bingwa mtetezi baada ya msimu uliopita kuchukua ubingwa huo kwa kuifunga Namungo mabao 2-1, fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Kocha huyo wa Yanga alitamba kuwa ubora wa kikosi chake umeanza kurejea na kumpa matumaini kuwa kilichoonekana ni kidogo, kwani msimu ujao mambo yatakuwa makubwa zaidi.

“Yanga imerudi na mwaka ujao mtaona wenyewe mambo mazuri yanakuja,”alisema.

Kabla ya fainali hiyo, Yanga itakuwa inakabiliwa na mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Ihefu itakayochezwa Julai 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na dhidi ya Dodoma Jiji utakayochezwa Julai 18, mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Chanzo: www.habarileo.co.tz