Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi ameendelea kukomaa na wapinzani wake Azam baada ya kuwafuata Kisiwani Unguja kuwasoma tena kwa mara nyingine.
Nabi amewafuata Azam kisiwani humo na kuwasoma kwa dakika 90 wakati matajiri hao wa Chamazi wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Jang'ombe katika Uwanja wa Amaan ukimalizika kwa suluhu 0-0.
Nabi ameonekana jukwaani akiwa na makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji wakiiangalia mchezo huo Azam ambayo imefanya usajili mkubwa msimu huu.
Nabi atakutana na Azam ya kocha Abdihamid Moallin katika mchezo wa tatu wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam Septemba 6, 2022.
Azam inataka kulipa kisasi dhidi ya Yanga baada ya kuchangia pointi 6 katika ubingwa wa Yanga msimu uliopita wakipoteza mechi zote mbili.
Kwenye ligi Yanga imeshinda mechi mbili huku Azam ikishinda moja na kutoa sare moja huku timu zote zikiingia katika mchezo wa tatu ambao unahesabiwa
Huo unakuwa mchezo wa pili kwa Nabi kuwasoma Azam ambapo mapema alikuwa jukwaani Agosti 14 wakati timu ikicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia.
Tayari kocha huyo amerejea jijini Dar leo kuishuhudia Taifa Stars ikicheza dhidi ya Uganda saa 10 jioni katika uwanja wa Mkapa.