Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi atoa msimamo kuhusu Doumbia

Doumbia Mamadou 1140x640 Doumbia

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Yanga wanataka kumuona beki wao mpya Mamadou Doumbia akikiwasha dhidi ya TP Mazembe.

Kocha Nasreddine Nabi amesema kuwa sio kila mchezaji anayesajiliwa na timu hiyo ataanza kucheza kwa haraka ambapo Doumbia anaendelea kupikwa taratibu kujua falsafa za timu hiyo.

Kocha Nabi alisema beki huyo ana ubora wake lakini changamoto pekee kubwa anayopambana nayo ni kuzoea kwanza falsafa za timu hiyo kuendana na mabeki wenzake wanaocheza.

“Nimeona watu wanaongelea sana kuhusu Mamadou (Doumbia), sio kila mchezaji akiletwa basi ataanza kucheza kwa haraka, huyu ni beki wa kati hili ni eneo ambalo unahitaji utulivu kumuingiza mtu mpya,”alisema Nabi.

“Tunafanya kazi kubwa sasa ya kumfanya Mamadou anazoea falsafa ya soka letu, wakati wake ukifika atacheza tu akishafanikiwa kucheza kama tunavyotaka.

“Tuna Lomalisa (Mutambala) nadhani watu wanaona bado kuna wakati tunamchezesha na kuna wakati anaweza asicheze lakini alipofika naye alisubiri kwanza na kuna wakati utafika Lomalisa atacheza sana.

“Huyu sio mshambuliaji ambaye anaweza kuja na ukampa nafasi haraka, hizi ni nafasi rahisi ambazo mchezaji anaweza kuja asubuhi na jioni ukaona uwezekano wa kumpa nafasi ya kucheza hata kwa dakika 20.”

Nabi alisema hata hivyo Doumbia anaendelea kuimarika kwa kushika baadhi ya mambo na uwepo wa mechi kubwa za karibu karibu pia umechangia kumchelewesha kuonekana ndani ya kikosi cha kwanza.

“Huwezi kumchukua Mamadou kuanza dhidi ya TP Mazembe kisa tumepoteza dhidi ya US Monastir itakuwa umemsababishia presha kubwa endapo akija kufanya kosa dogo, ndio maana tulianza kumpa nafasi taratibu.”

Tangu atue Yanga Doumbia amecheza dakika 45 pekee za mechi ya mashindano alipoingia kipindi cha pili wakati Yanga ikiifunga Rhino ya Tabora kwa mabao 7-0, kwenye mchezo wa Kombe la Azam Shirikisho uliofanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live