Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi atoa ahadi kwa Mashabiki, watokee kwa Mkapa

Nabi Pic Data Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi, amewaeleza mashabiki wa timu ya Yanga kuwa, wajitokeze kwa wingi kwani burudani itaendelea pale ilipoishia ndani ya kikosi hicho.

Katika ujumbe alioutuma kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Hassan Bumbuli, Nabi amesema hawana shaka na aina ya soka lao ambalo ni kivutio kwa mashabiki wao.

"Kocha hakuweza kwenda kufanya press ya kabla ya mechi pale TFF, lakini maagizo yake kwa Wanayanga ni kwamba waje kwa wingi, kushuhudia burudani walizozizoea" amesema bumbuli

"Huo ndio ujumbe alionituma niufikishe kwenu sasa sisi kama Yanga, tunajua namna tunavyoburudika na soka letu kiasi wengine wanapenda tucheze kila siku"

Yanga majira ya saa 12 jioni ya leo watawakaribisha Maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live