Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi arejea mzigoni Morocco, vipi kuhusu dili la Kaizer Chiefs?

Kocha Nabi Msz Nabi arejea mzigoni Morocco

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

AS FAR imeanza na mazoezi leo baada ya kupoteza taji la ligi Kuu ya Morocco (Botola) dhidi ya Raja wiki iliyopita.

FAR wataanza maandalizi ya mchuano wao wa nusu fainali ya Throne Cup dhidi ya Maghreb Fez siku ya Jumapili.

Nasreddine Nabi atakuwepo na ataendelea kuwa mtaalamu lakini tayari ameamua kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho nchini Morocco.

Zipo taarifa zinaeleza kuwa, Nabi amemaliza mazungumzo na muda wowote atasaini mkataba na Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini baada ya kufanya vibaya Morocco.

Kaizer imekuwa kwenye mawindo kuitaka saini ya Mtunusia huyo ikimfatilia pindi alipokua akiifundisha Yanga lakini walishindwana vitu vichache.

Je, tutegemee kuuona ufalme mpya wa nabi Afika Kusini?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live