Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi apumzisha wanne, aifungia kazi Kagera Sugar

C7B366CD 8F0C 45CF B96C 3BEA90C265F6.jpeg Kibwana Shomari anaanza mchezo wa leo sambamba na Zawadi Mauya

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Yanga, Nasredinne Nabi amewapumzisha mastaa wanne walioanza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika walioshinda kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Yanga itavaana na Kagera Sugar muda mfupi ujao katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaoanza saa 10:00 jioni.

Mastaa waliopumzishwa leo ambao walianza dhidi ya Club Africain ni Bernad Morrison, Jesus Moloko, Khalid Aucho na Yanick Bangala huku Kocha Nabi akiifungia kazi Kagera Sugar akianza na mabeki wa kati watatu na washambuliaji wawili.

Nabi ameingia na mfumo wa 3-5-2 ambapo langoni ameanza na kipa, Djigui Diarra, mabeki wa pembeni Kibwana Shomari na Joyce Lomalisa huku mabeki watatu wa kati wakiwa ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Ibrahim Bacca.

Viungo ni Zawadi Mauya, Salum Abubakar 'Sureboy' na Feisal Salum 'Feitoto' huku washambuliaji wakiwa ni Fiston Mayele na kinda Clement Msize.

Wachezaji wa akiba ni; Abuutwalib Mshery, Yanick Bangala, Djuma Shaban, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Bernad Morrison, Yusuph Athuman, Farid Mussa na Tuisila Kisinda.

Chanzo: Mwanaspoti