Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi apewa saa 48 tu Kaizer Chiefs

Nabi Kubaki Yanga Nabi apewa saa 48 tu Kaizer Chiefs

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema ndani ya saa 48 mustakabali wake na Kaizer Chiefs utakuwa umejulikana.

Kaizer Chiefs imekuwa ikitajwa muda mrefu kuwa inamtaka kocha huyo, lakini jana akihojiwa na The South African alisema mazungumzo yanaendelea na ndani ya saa 48 watakuwa wameshamalizana.

“Kwa sasa ni ngumu kukupa taarifa, lakini tambua kuwa tunaendelea kuzungumza na viongozi wa Chiefs kupitia wakala wangu na ndani ya saa 48 tutakuwa tumeshakamilisha na kufahamu nini kinaendelea,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live