Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi apagawa Yanga, Mazembe waondoka na jina la Bangala

YANGA BANGALA NABIII.jpeg Bangala na Nabi

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mashabiki wa Yanga wakitamba mtaani kwa ushindi wao wa kwanza dhidi ya TP Mazembe kocha wao Nasreddine Nabi amefichua simulizi nzito ambayo bado akiikumbuka anakosa majibu kutoka kwa wachezaji wake.

Yanga juzi iliichapa Mazembe kwa mabao 3-1 ukiwa ndio ushindi wao wa kwanza dhidi ya klabu hiyo lakini pia matokeo hayo yanaipa pointi tatu za kwanza katika mechi za Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa wakishika nafasi ya pili katika kundi lao D.

Nabi alisema kitu pekee ambacho bado anajiukiza katika akili yake ni kukumbuka jinsi wachezaji wake walivyokuwa wanataka kucheza mechi hiyo huku wakimwambia kwamba watashinda dhidi ya Mazembe.

Nabi alisema yeye na wasaidizi wake walikuwa katika wakati mgumu kuamua nani ataanza katika mchezo huo kufuatia morali ya juu ambayo wachezaji walikuwa nayo ikiwa ni tofauti tangu apewe ajira ya kuifundisha Yanga.

"Kipindi chote cha maandalizi kilikuwa ni kipindi cha maajabu, kila mchezaji alikuwa anataka kucheza hii mechi, wako wachezaji walikuwa wananipigia mpaka simu wakiniomba kocha nifikirie nicheze hii mechi Yanga tunashinda,"alisema Nabi.

"Kuna mchezaji alinifuata na kuniomba nimpange nafasi tofauti na ambayo tunampanga, na wote wanakwambia tunakwenda kushinda lakini hata mazoezini kulikuwa na morali ambayo sidhani kama nimewahi kuiona tangu nifike hapa Yanga.

"Hii ni maana kwamba wachezaji walijua walikosea wapi kule Tunisia na walitaka kurudisha tabasamu kwa mashabiki wao na viongozi, hata tuliposhinda walinifuata na kuniambia kocha watu wetu wameefurahi.

Aidha Nabi aliongeza kuwa ushindi huo unakwenda kurudisha heshima sio tu Tanzania Bali Afrika wakithibitisha kwamba hawakuifunga Club Africain kwao kwa kubahatisha.

"Tuna timu bora changamoto zilizopo jukumu kubwa ni kuzikabili na kutafuta akili mpya,wapo ambao walidhani Yanga ilibahatisha kushinda mbele ya Club Africain, hii inathibitisha kwamba tuna kikosi imara sio tu hapa ndani bali hata Afrika tunahitaji heshima kwa kiwango chetu.

USIKIE UONGOZI

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji ameongeza kuwa ushindi ambao wameupata mbele ya Mazembe ni gia ya kuanza safari yenye kasi kupata ushindi zaidi.

Arafat alisema baada ya Mazembe sasa wanawataka wachezaji wao kuigeukia mechi ya Ligi dhidi ya KMC na kushinda vizuri kabla ya kuanza hesabu zingine za kuwafuata Real Bamako ya Mali, katika mechi yao ya tatu ya hatua ya makundi.

"Tulikuwa na Imani kubwa na kauli za wachezaji wetu, kila tulipozungumza nao walisema wanaisubiri Mazembe kazi wamemaliza,"alisema Arafat

"Sasa kazi inayofuata ni kukimbia zaidi, hii ni gia ya kuondokea safari inaanzia hapa anayefuata Sasa ni KMC tumewaambia wachezaji tunatakiwa kuendeleza moto wa ushindi wetu.

"Uongozi tuko mbali tunacheza ligi na wengine wameshaanza hesabu za kuwafuata Real Bamako tunataka kwenda kushinda kule,tunajua na wachezaji wanajua walikosea wapi tulipokwenda Tunisia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live