Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aoneshwa udhaifu wa Yanga

Saido Pic Saido Ntibanzokiza

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametonywa mapema kuhakikisha anafanya kazi ya ziada kwenye kuboresha upigaji wa mipira iliyokufa ili kupata mabao mengi zaidi kwenye kila mchezo.

Jambo hilo lilitokana na mchezo wao wa 16 bora kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Biashara United kupata nafasi nyingi za mipira ya kona na frii-kiki lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo.

Winga wake Saido Ntibazonkiza ndiye aliyekuwa anahusika kwenye kupiga mipira hiyo kwenye mchezo huo lakini hakuwa kwenye kiwango kizuri akishindwa kutumia mipira hiyo ya adhabu.

Katika kona 11 ambazo walipata kwenye mchezo mzima huku Biashara Utd wakipata kona moja tena kwenye kipindi cha pili, Ntibazonkiza alipiga kona zote huku moja tu ya dakika 21 ndiyo ilizaa bao la kwanza alilofunga Yanick Bangala ambalo lilitokana na kipa kuutema mpira kisha yeye alipiga krosi tena na kupigwa kichwa na Bakari Mwamnyeto na kugonga mwamba kisha Yanick Bangala alipiga kichwa ukachezwa na kipa wa Biashara na ulipotua chini Mcongo huyo aliupiga na kwenda wavuni.

Saido pia alipiga frii-kiki kadhaa ikiwamo ya dakika 45 baada ya kiungo Khalid Aucho kufanyiwa madhambi nje kidogo ya boksi lakini akapaisha, na alikosa pia frii-kiki nyingine nje ya boksi katika dakika 62 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya boksi.

Licha ya kukosa ‘frii-kiki’ nyingi na kupiga kona ambazo hazikuzaa mabao, Ntibazonkiza alihusika kwenye bao la pili dakika 29 baada ya kuwatoka mabeki wa Biashara United na kupiga pasi kwa Fiston Mayele aliyeuweka mpira wavuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live