Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi anaongoza Ligi Kuu ya Morocco

Nabi Msfg Nabi anaongoza Ligi Kuu ya Morocco

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la Hatim Essaoubi dakika ya 84 limetosha kuwapeleka kileleni mwa msimamo wa Botola Pro vijana wa Kocha Nasredine Nabi.

Ushindi huu unawafanya FAR Rabat wafikishe alama 14 sawa na RS Berkane na FUS Rabat, lakini wao wanakaa kileleni kutokana na kuwa na faida ya kufunga mabao mengi zaidi.

Berkane wamefunga mabao 10 na kuruhusu matatu huku FAR Rabat wakifunga mabao 12 na kuruhusu mabao matano, wote wana +7 lakini ASFAR wamekaa kileleni Kwa sababu wamefunga mabao mengi zaidi.

Msimamo wa Ligi Kuu ya Morocco ni kwamba, tofauti ya anayeongoza Ligi na anayeshika nafasi ya 8 pale ni alama nne tuuu.

Ikumbukwe kuwa, kabla hajacheza mchezo huo, Nabi na timu yake walikuwa nafasi ya sita ya Ligi, hivyo mchezo mmoja tu umewapeleka mpaka nafasi ya kwanza.

Licha ya kwamba ASFAR ndiye Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya Morocco, lakini kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Nabi ameshindwa kuivusha kwenda hatua ya Makundi baada ya kutolewa na timu ya nyumbani kwao Tunisia, Etoile Du Sahel kwa kufungwa bao 2-1 nyumbani kwao kisha wakafungwa tena 1-0 ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live