Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi amvulia kofia Gamondi "Yanga itafika fainali CAFCL"

Nabi Gamondi Msz Kocha Gamondi na Nabi.

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Nasreddine Nabi amekiri kuwa ubora wa Klabu ya Yanga umeongfezeka na imekuwa timu bora zaidi Barani Afrika kwa sasa.

Nabi ambaye amewahi kuinoa Yanga kwa misimu miwili na kubeba makombe yote ya ndani huku akifanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kutimkia FAR Rabat ya Morocco, amesema kuwa Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kufika fainali.

"Tumestaili ichi kilicho tupata niliutambua ubora wa yanga maana mimi ndo naijua na nimeifundisha, wana kikosi bora sana na hakijashuka kiwango toka niache hadi leo.

"Nimefungwa kwa ubora wa wachezaji hasa Azizi Ki na Mzize niliwambia wachezaji wangu hao watu wawachunge ila ndo ivyo tumeadhibiwa. Yes nimepewa timu nina wiki tatu sasa bado naijenga kimfumo zaidi na naitaji waniongezee wachezaji wengine wenye quality zaidi.

"Naiona Yanga msimu ujao kimataifa ikifika Fainali club bingwa nisiwe mnafki wana timu bora sana hasa safu yao ya ushambuliaji wakatili sana, Yes kwa mchezaji niliyevutiwa naye kwa yanga yule Maxi na Aziz KI natamani sana ningekua nao kwenye kikosi changu," amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: