Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi amtumia mamadou Doumbia kuwavuruga Bamako

DOUMBIA YANGA WE.jpeg Nabi amtumia mamadou Doumbia kuwavuruga Bamako

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amefichua kuwa, uwepo wa beki mpya wa timu hiyo, Mamadou Doumbia raia wa Mali, utawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata ushindi katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Real Bamako.

Nabi ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo wa Kundi D unaotarajiwa kupigwa Februari 26, mwaka huu nchini Mali, ikiwa ni baada ya kuwachapa TP Mazembe mabao 3-1, juzi Jumapili.

Yanga kabla ya kuelekea Mali kucheza na Real Bamako, kesho Jumatano itapambana na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Nabi alisema kuwa, licha ya uwepo wa kipa Djigui Diara raia wa Mali ndani ya kikosi chake, lakini anaamini Doumbia atawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili kufikia malengo ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

“Tumemaliza kazi ya hapa nyumbani, lakini bado tuna kibarua kizito cha kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri katika mchezo ujao, tutawatumia wachezaji wetu kutoka Mali, Doumbia na Diara ili kupata matokeo mazuri.

“Wapinzani wetu siyo timu ya kubezwa kwa sababu tumewafuatilia na tutaendelea kufuatilia mechi zao ili kupata namna bora ya kupata ushindi wa ugenini kwa sababu ukiangalia hawa tulionao watatusaidia sehemu kubwa kupata ushindi kule Mali japo kwa sasa tunarudisha malengo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live