Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi amshangaa Dickson Job

Nabi Job Tr Nabi amshangaa Dickson Job

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALiyekuwa Kocha Muu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameonyesha kushangazwa na uwezo mkubwa alio nao beki kisiki wa timu hiyo, Dickson Job ambaye amekuwa akimudu nafasi mbalimbali anazopangwa kucheza na kutimiza vyema majukumu yake ndani ya Timu.

"Kama kuna mchezaji aliyenishangaza juu ya kipaji chake basi ni Dickson Job, wakati nafika na nilipoambiwa anacheza beki wa kati nilisubiri kuona ana kitu gani cha ziada lakini alinijibu kwa vitendo uwanjani.

"Huyu ni kijana mdogo ambaye ana akili kubwa sana anapokuwa uwanjani, Job hajui kukataa jukumu unalomtuma amekuwa ni rahisi kwake kubadilika wakati wote kocha ukimtaka kufanya hivyo.

"Ana nidhamu kubwa ni sawa na wale rafikizake Kibwana (Shomary) na mwanangu Mshery bahati mbaya aliumia lakini ni kipa mzuri, kwa Job ni bahati mbaya sana anacheza soka Tanzania,” amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: