Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi ampa somo zito Aziz KI, msala wa Dabi umekaaje?

Aziz Ki Yanga Hat Stephen Aziz KI alifunga bao la kusawazisha katika Dabi iliyopita

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Haya ndio maajabu ya Stephane Aziz KI. Wakati ambao wadau na mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiona kiwango chake kimeshuka kwa vipindi tofauti, nyota huyo wa Kimataifa kutoka Burkina Faso amekuwa akiibuka na kuwashangaza kwa kufanya makubwa.

Ni nani ambaye alijua atauwasha vile kwenye mchezo uliopita wa Yanga wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar? Unakumbuka kilichotokea dhidi ya Club Africain kule Tunisia wakati wakipigania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na vipi kuhusu mchezo wa kwanza wa dabi msimu huu kwenye Ligi.

Wakati ambao Aziz Ki anajitafuta amekuwa na maajabu yake na kile kilichotokea dhidi ya Kagera kwa kufunga hat trick ya kwanza akiwa na Yanga ilikuwa ni muendelezo tu wa kile ambacho amefanya kwa nyakati tofauti, jambo lililomfanya Kocha Nasreddine Nabi kuchekelea.

Akizungumzia kurejea kwa kiwango cha Aziz KI, kocha Nabi alisema kikao ambacho walifanya na mshambuliaji hiyo kimechangia juhudi kubwa za kutaka kuona anarudi katika kiwango chake. Nabi alisema Aziz KI anatakiwa sasa kuendeleza moto wa kufunga na kucheza vizuri.

"Tulifanya juhudi kubwa ya kuongea naye na kumuelewesha jinsi anavyotakiwa kurudi katika kiwango chake, mimi binafsi niliongea naye lakini pia wasaidizi wangu na hata viongozi nao walikuwa wakifanya hizi juhudi," alisema Nabi.

"Tulikuwa tunaumia mioyo yetu kumuona anakuwa katika wakati mgumu licha ya jina lake kubwa, nafikiri sasa amepata sehemu ya kuanzia na kuendeleza makali yake ili azidi kufanya makubwa zaidi."

Aziz ndiye aliyeipeleka Yanga katika hatua ya makundi kwa kufunga bao pakee, Tunis dhidi ya Africain lakini pia kama unakumbuka wakati alivyopoa aliibukia kwenye dabi na kuisawazishia Yanga kwa shuti kali la faulo wakati wakitoka sare (1-1) dhidi ya Simba.

Chanzo: Mwanaspoti