Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi ampa Makambo mfupa mgumu Yanga

Makambo Heritier Ebenezer Heritier Makambo

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Yanga wamegawanyika wapo wanaona mshambuliaji wao, Heritier Makambo hakucheza vizuri mchezo dhidi ya KMC na Geita Gold alizoanza kikosi cha kwanza wengine wakiona alikuwa sawa, lakini kocha wake amemaliza ubishi huku akitoa msimamo wake.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amesea kuwa Makambo hakuwa sawa mechi hizo kutokana na kutokucheza kwa muda mrefu, lakini amemtaka kuanza kujiandaa kucheza zaidi kwa kuwa sasa anatakiwa kuthibitisha ubora wake kwa kushindana na straika mwenzake Fiston Mayele.

Kocha huyo alisema Makambo anatakiwa kuanza kutumia nafasi ya muda atakaokuwa anampa kufunga ili kumpa changamoto Mayele ambaye amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga.

“Sioni kama alicheza vibaya (Makambo) ila sema hakuwa na bahati ya kufunga. Hakuna timu inayomtegemea mtu mmoja, kila mchezaji yuko hapa kushindana ili aitumikie Yanga, Makambo anatakiwa kurudisha kujiamini kuanzia mazoezini ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara,” alisema Nabi na kuongeza;

“Namuhitaji Makambo ampe changamoto Mayele, niko tayari kumpa muda zaidi kama atakuwa na mwendelezo wa kuonyesha ubora zaidi hii ni timu ambayo kila mmoja ana nafasi kitu kilichobaki ni juhudi za mchezaji mwenyewe kupigania namba.”

Makambo alianzishwa kwenye mechi hizo zilizoisha kwa Yanga kushinda bao 1-0 kila mchezo na kuifanya ikae kileleni mwa msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 20 baada ya mechi nane na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza katika ligi tangu Aprili 25 mwaka jana idadi ikifika mechi 45.

Chanzo: Mwanaspoti