Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi akomaa na Mwamnyeto Yanga

Nondo Mayele Nabi akomaa na Mwamnyeto Yanga

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kuna idara mbili zimekomaliwa kambi ya Yanga kabla ya timu hiyo kushuka Uwanjani Jumapili kumalizana na Rivers United ya Nigeria lakini kocha wao kuna kauli kaitoa ambayo itamfanya kila shabiki wa Yanga kuwahi mapema uwanjani.

Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi yao yanayofanyika jioni pale Avic Town na kama unataka kujua kipi kinapikwa huko basi tambua makocha wa timu hiyo wamekomaa na idara mbili kubwa za ulinzi na ile ya ushambuliaji.

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze wamekuwa wakali kwenye mchezo huu kwa kuwa wameona kama wachezaji wanaweza kubweteka kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza nchini Nigeria.

Nabi na wasaidizi wake wakuwa wakifanya mazoezi mbalimbali kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kubwa kwenye eneo la ulinzi ambalo li[o chini ya Bakari Mwamnyeto, Dckson Job, Joyce Lomalisa na Djuma Shaaban ili kuhakikisha hawaruhusu bao lolote kwenye mchezo huu.

Wachezaji wa Yanga wamekuwa wakipokea maelekezo mengi ya mdomo lakini pia hata vitendo kuhakikisha wanakuwa na ubora wa kuwazima washambuliaji wa Rivers ambao Nabi anasema wana uwezo mzuri uwanjani.

Wachezaji hao wametakiwa kusisitizana wakati wa kupiga mipira ya adhabu ndogo, krosi na hata kona kuhakikisha kila mmoja anapambana na mtu wake kwa ukamilifu na sio kuzuga huku wakitakiwa kukumbushana kila wakati wakiwa uwanjani.

Eneo lingine ambalo limekuwa likikomaliwa ni ile idara ya kufunga mabao ambapo washambuliaji wa timu hiyo wamekuwa wakipewa mbinu za kutegua mitego ya mabeki wa Rivers.

Mazoezi hayo ya washambuliaji yamekuwa yakifanyika kwa muunganiko na viungo washambulaiji wa kati na hata wale wa kutokea pembeni kuhakikisha kila shambulizi linalofanyika kuna kuwa na athari kwa wapinzani wao.

Mshambuliaji Fiston Mayele ndiyo pekee ana uhakika wa kuanza kufuatiwa kufanya vizuri mazoezini lakini pia akibadilishiwa wenzake mbalimbali akiwemo Kennedy Musonda, Clement Mzize na hata Stephane Aziz KI na Jesus Moloko pembeni. Kocha wa Yanga Nabi ameliambia Mwanaspoti kuwa wako katika siku nne za moto mazoezini kabla ya mchezo wa Jumapili Aprili 30, wakitaka kujiweka tayari kuwang'oa Rivers kwa ushindi mwingine nyumbani.

Nabi aliongeza kuwa anaridhika na morali ya wachezaji wake akiwathibitishia mashabiki kwamba kila mchezaji aliyeko kambini amekuwa katika mzuka mkubwa wakiitaka mechi hiyo ambayo inaweza kuwavusha kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

"Tunataka kuwa na dakika tisini mpya ambazo tutakuwa imara katika ulinzi lakini pia kufunga mabao mengine tupate ushindi na hapa nyumbani, hakuna njia nyingine ya kutuhakikshia kufuzu kama hatutakuwa tayari kushinda hapa kwetu,"alisema Nabi.

"Nafurahi kuona morali ya wachezaji iko juu sana tofauti na huko nyuma naweza kusema morali hii ni kama ile tulipocheza na TP Mazembe hapa, kila mchezaji anaonyesha yuko tayari kupewa nafasi hili ni muhimu sana kwa timu yetu," alisema Nabi.

Chanzo: Mwanaspoti