Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aingia kinyang'anyiro cha Kocha Bora Afrika

Nabi Kocha Afrika Nasreddine Nabi

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga SC ,Nasreddine Nabi ameorodheshwa na Mtandao wa Foot-African.com kwenye orodha ya Makocha waoanowania Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Afrika.

Msimamo ulivyo mpaka sasa

1. Walid Regragui (Morocco): 36%

2. Aliou Cissé (Sénégal): 29%

3. Abdelhak Benchikha (USM Alger): 21%

4. Nasreddine Nabi (Young Africans): 13%

Nabi akiwa Kocha wa Yanga msimu uliopita alikuwa na mafanikio makubwa akibeba Ngao ya Jamii, Kombe la Azam Sports Federation, Ligi Kuu na kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nabi kwa sasa hana timu baada ya kuachana na Klabu ya Yanga mwishoni mwa msimu uliopita.

Mwananchi unaweza kumpigia kura Nasreddine Nabi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live