Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasteddine Nabi amesema mazungumzo na klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika zkusini yamemalizika bila muafaka.
Nabi ametoa kauli hiyo baada ya kushindwana na klabu hiyo iliyokuwa ikimtaka na kuamua kuchukua kocha mwingine baada ya pande zote mbili kutofikia maridhiano ya kile ambacho kila mmoja alikitaka.
"J informe mes chers amis que les négociations avec kaiser cheefs ont pris fin sans arrivé à un accord final .la principale raison est le refus de mon staff technique.je remercie les dirigeants de ce prestigieux club pour leur intérêt et lui souhaitons tout le meilleur." - Nasreddine Nabi
Kwa tafsiri;
"Napenda kuwajulisha wapendwa rafiki zangu kuwa, makubaliano na Kaizer chiefs ???????? yamemalizika bila kufikia muafaka. Sababu kuu iliyopelekea hilo ni klabu kutokubali benchi langu la ufundi.
"Nawashukuru viongozi wa klabu (Kaizer chiefs) kwa kuonesha nia ya kunihitaji na nawatakia kila lakheri," amesema Nasreddine Nabi.