Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aendeleza ubabe Morocco

Nasreddine Nabi Msiba Nabi aendeleza ubabe Morocco

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi ameendeleza rekodi nzuri katika kikosi cha FAR Rabat ya nchi hiyo baada ya juzi kushinda mabao 5-0, dhidi ya Mouloudia Oujda na kukaa kileleni mwa msimamo akifikisha pointi 43 kufuatia michezo 19.

Ushindi huo umemfanya kuziacha vigogo wawili wa nchi hiyo Raja Casablanca yenye pointi 41 na Wydad Casablanca yenye 31, zote zikicheza michezo 19.

Kocha huyo ambaye aliifikisha Yanga kwenye hatua ya Fainali Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kuongoza ila ameshindwa kutamba na timu hiyo kimataifa kwani alijikuta akiondolewa mapema hatua ya mtoano baada ya kushinda mechi mbili kati ya nne.

Nabi aliondoka nchini akiwa tayari ameipa Yanga mataji mawili ya Ligi Kuu Bara mfululizo na taji moja la ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Pia aliiongoza Yanga kucheza michezo 48 ya Ligi Kuu Bara bila kufungwa ambapo kati ya hiyo alishinda 36 na kutoka sare 12 huku akiachana na kikosi hicho msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Muagentina, Miguel Gamondi Juni 24, mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live