Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi acharuka: Sitaki usiniulize kuhusu Robertinho

Nabi Robertinho Er Nabi na Robertinho

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasredinne Mohammed Nabi amecharuka kufuatia mwandishi mmoja wa habari kumhoji kuhusu kuwa kibonde kwa kocha wa Simba, Robertinho ambaye amemfunga mara mbili baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya Simba.

Ikumbukwe kuwa, Robertinho ameifunga Yanga katika katika mchezo wa Siku ya Wananchi kwa bao 2-0 akiwa na Vipers, kisha mechi ya jana akiwa na Simba bao 2-0.

"Nawapongeza Simba SC kwa ushindi, japokuwa goli la kwanza lililosababishwa na kona, ile kona haikuwa halali lakini muamuzi akaamua iwe kona hata ukiangalia kwenye TV utaona hili, matukio kama haya yanawatoa wachezaji kwenye hali ya mchezo.

"Kipindi cha pili tulijitahidi kurudi kwa nguvu tukatengeneza nafasi lakini hatukufanikiwa, lakini nawapongeza Simba wamepata magoli ndani ya dk 90 na wameshinda mchezo.

"Yanga imecheza na Simba haijacheza na Robertinho, mechi ya kirafiki ni tofauti na mechi ya ushindani, unazungumzia mechi ya Vipers mwaka mzima uliopita, nini? Refa ametoa kona kwa Simba haikuwa kona.

"Ukininuliza niulize kuhusu Yanga, Simba, usiniulize kuhusu Nabi, Robertinho sijui Mourinho mimi sijui. Nenda moja kwa moja fresh? Siwezi ku-appreciate, ni-appreciate kwa kipi? Msimu mzima tunaongoza ligi, kwa mpira upi appreciate, sisi ni mabingwa huu msimu.

"Tazama bao la kwanza. Lakini ninahitaji marefa walio makini, marefa wacha Mungu, wenye hofu na Mungu. Tunataka marefa professional. Unifokee, kwa sababu ukinifokea utanifungua yote," amesema Kocha Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: