Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi, Yondani wafungiwa mechi tatu

Nabi YOND Nabi, Yondani wafungiwa mechi tatu

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Aprili 21, 2022 imepitia taarifa za Kamishna, Waamuzi na taarifa nyingine zilizokusanywa katika michezo mitatu ya robo fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) iliyochezwa.

Mchezo namba 89 (Young Africans v Geita Gold) Katika mchezo huo uliochezwa Aprili 10, 2022 uwanja wa Benjamin Mkapa, Mwamuzi Raphael Ikambi alishindwa kutafsiri ipasavyo sheria za mpira wa miguu kwenye baadhi ya maamuzi yake kinyume na kanuni ya 42:1 inayohusu Udhibiti wa Waamuzi, Kamati inapeleka shauri lake kwenye Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.

Mchezaji Kelvin Yondani wa Geita Gold alimkanyaga kwa makusudi mchezaji Fiston Mayele wa Young Africans bila ya kuwa na mpira kinyume na Kanuni ya 41:5:2 inayohusu Udhibiti kwa Wachezaji, Kamati imemfungia Kelvin Yondani kucheza michezo mitatu (3) na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) kwa kosa hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5:2 ya Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2021.

Kocha Mkuu wa Young Africans Mohamed Nabi alitolewa kwa kadi nyekundu na Mwamuzi wa mchezo kwa kosa la kuwashabulia kwa lugha ya matusi Waaamuzi wakati wakitimiza majukumu yao kinyume na Kanuni za Mashindano.

Kamati ilijiridihisha kuwa alitenda makosa ya kinidhamu kinyume na utaratibu wa Kanuni za Kombe la Shirikisho (ASFC), alikiuka kanuni ya 45:2:1 juu ya Udhibiti wa Makocha, Kamati imemfungia Kocha Mohamed Nabi kuingoza timu yake kwenye vyumba vya kuvalia na benchi la ufundi katika michezo mitatu (3) inayofuatia ya timu yake na kutozwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa mujibu wa Kanuni ya 45:2:11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live