Kuelekea mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF, dhidi ya Monastir siku ya leo, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi na mshambuliaji Fiston Mayele wamefanya mahojiano na Waandishi wa habari.
Mkutano huu na waandishi wa habari umefanyika kwenye ukumbi wa ndani ya uwanja wa Olympic Rades ambapo mchezo huo utapigwavmajira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
KUHUSU MAANDALIZI
“Nawapongeza sana viongozi wa Yanga kwa kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri hapa Tunisia. Tumekuwa na kambi nzuri sana hapa na vijana wako kwenye hali nzuri.
“Kuhusu maandalizi sisi tulishaanza tangu tukiwa Dar Es Salaam, tumefanya maandalizi mazuri na vijana wako tayari kwa ajili ya mchezo huu.
”Ni mchezo muhimu kwetu katika safari yetu ya kutafuta tiketi ya kwenda Robo Fainali ya michuano hii msimu huu,” alisema Nabi.