Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Vijana wapo tayari kuandika historia kesho

AZIZ NA NABII Nabi: Vijana wapo tayari kuandika historia kesho

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohammed Nabi amesema kuwa katika mchezo wa kesho dhidi ya Rivers United, hatapaki basi badala yake atashambulia na kujilinda kwa tahadhari ili asiruhusu timu yake kufungwa.

Mauya amesema hayo leo Jumamosi, Aprili 29, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao wa marudiano wa robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

“Tuna furaha kwa hatua tuliyofikia Kombe la Shirikisho, benchi la ufundi, wachezaji pamoja na uongozi wa klabu, sote akili yetu ipo kwenye mchezo wa kesho, tumejiandaa vizuri. Licha ya kupata matokeo mazuri ugenini hii haitufanyi tujiamini na kushindwa kupeleka mawazo yetu kwenye mchezo wa kesho.

“Mpira una historia usipoifuata utakuwa sio mtu wa mpira, zipo timu ziliwahi kushinda ugenini wakaja kutolewa nyumbani, sisi hayo yote tulijifunza sababu ndio mpira na tukayafanyia kazi.

“Wachezaji wangu wana ari kubwa ya kupata ushindi kwa sababu wiki nzima tangu turudi kutoka Nigeria wanajituma, wanafanya mazoezi vizuri na morali ipo juu kupambana ili kesho tupate matokeo.

“Benchi la ufundi na wachezaji tumekaa na kusema kuwa mechi haijaisha licha ya vyombo vya habari kuandika kwamba tumeshafuzu, lazima tupambane pamoja ili tupate matokeo ya kutupeleka hatua inayofuata,” amesema Nabi.

Yanga wakiwa na mtaji wa bao 2-0, watakuwa na kibarua kigumu kesho wakishuka katika dimba la Mkapa kukipiga na Rivers United wakisaka tiketi ya kusonga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: