Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Marumo wamekwisha

NABI MAYELE NA AZIZ Nabi: Marumo wamekwisha

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wamekwisha! Ndivyo unaweza kusema baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi kuweka wazi kila kitu kipo tayari kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Marumo Gallants leo pale Afrika Kusini.

Mchezo huo utakaopigwa Dimba la wa Royal Bafokeng saa 1:00 usiku kwa saa za Bongo ni wa marudiano baada ya ule wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar kuisha kwa Yanga kushinda mabao 2-0.

Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga kilichoanza kilikuwa; Djigui Diarra, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Yannick Bangala, Jesus Moloko, Khalid Aucho, Fiston Mayele, Aziz Ki na Tuisila Kisinda sasa Nabi amepanga kufanya mabadiliko kidogo kueleka mchezo wa leo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Nabi alisema kuwa: “Kutakuwa na mabadiliko katika kikosi ambacho kimetoka kucheza mchezo wa kwanza kuelekea katka mchezo wetu huu wa pili ambao ni mchezo wa marudiano.

“Kuna tofauti kubwa sana katika mchezo wa kwanza na ule mchezo wa pili, kuna vitu vingi sana ambavyo hubadilika haswa pale ambapo timu inacheza ugenini tena katika hatua kubwa kama hii.

“Mara nyingi mabadiliko ya mbinu na vitu vingine hutokea, kikubwa wote ni wachezaji wa Yanga na tunaamini kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya kuipa ushindi Yanga na kuipambania timu iweze kufanya vizuri.”

WACHEZAJI WANAZITAKA MEDALI ZA CAF Wakati huohuo, wachezaji wa Yanga tangu wamefika nchini Afrika Kusini wamekuwa wakifanya vikao hotelini kwa lengo la kuhimizana na kupeana morali ya kupambana uwanjani kwa lengo la kutimiza malengo ya kufuzu hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa kambi yao inakwenda vizuri na wachezaji wana hamasa ya hali ya juu na kikubwa wanataka kuandika historia ya kuvaa medali za Caf katika msimu huu.

Kamwe alisema kuwa tangu msafara wa timu hiyo umetua Afrika Kusini, wachezaji wao wameonekana kufanya vikao vya kuhimizana kupambana kwa yule atakayepata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

“Kama uongozi tunafurahia kuona wachezaji wetu wote wakihimizana kupambana kwa kila atakayepata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na kikubwa kupata matokeo mazuri ya ushindi ili waandike historia ya kuvaa medali za Caf msimu huu.

“Uzuri kila mchezaji anaitaka mechi hii na kwa lengo la kutaka kuandika historia, tunaamini haitakuwa mechi nyepesi kwetu kwani wapinzani wetu nao wamepania kupata jushindi hapa nyumbani kwao.

“Na tangu tumefika hapa jana (juzi) timu chini ya Kocha Mkuu Nasreddine (Nabi) imefanya mazoezi mara mbili Jumapili na Jumatatu kwa maana ya asubuhi na jioni pekee.

“Lakini leo (jana Jumanne) tumefanya program moja pekee ya mazoezi ya jioni kwenye uwanja ambao tutakaoutumia katika mchezo huo,” alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: