Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi Kufanya Uamuzi Mgumu Yanga

Yacouba Sogne Nabi Kufanya Uamuzi Mgumu Yanga

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Yanga kwa kushirikiana na Benchi la Ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, huenda wakafanya uamuzi mgumu wa kuliondoa jina la Mburkinabe, Yacouba Songne na kumuingiza winga mwingine mpya.

Hiyo ni katika kuimarisha kikosi hicho kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo ambalo lilifunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kutarajiwa kufungwa Januari 15, 2022.

Yacouba kwa sasa yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha ya goti aliyoyapata Novemba, mwaka huu na tarayi amepatiwa matibabu nchini Tunisia.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amesema kuwa, kutokana na ukubwa wa jeraha ambalo amelipata Yacouba, huenda mshambuliaji huyo akakosekana msimu mzima, hivyo benchi la ufundi linafikiria kuliondoa jina lake katika wachezaji itakaowaumia na kumsajili mwingine.

Aliongeza kuwa, licha ya kuliondoa jina la Yacouba, lakini mshambuliaji huyo ataendelea kuwepo katika timu hiyo, huku akilipwa mshahara wa kila mwezi akisubiri kupona.

“Yacouba mwenyewe anafahamu kila kitu kuhusiana na jina lake kuondolewa katika orodha ya wachezaji wa kigeni waliokuwepo Yanga.

“Uongozi upo katika mazun– gumzo na baadhi ya viungo washambuliaji kutoka nchini DR Congo baada ya kumalizana na Chico (Ushindi) kutoka TP Mazembe.

“Hivyo licha ya Yacouba kuondolewa, lakini ataendelea kubaki Yanga hadi atakapopona na katika kipindi chote atakuwa akipokea mshahara wa kila mwezi,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia usajili, Nabi alisema: “Ripoti yangu niliyowapa viongozi imeagiza kusajili wachezaji wanne, kati ya hao yupo beki wa kati, kiungo, mshambuliaji na winga.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live