Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi, Kaze wakusanya mafaili ya Dodoma Jiji

Nabi Kaze Uhuruu Nabi, Kaze wakusanya mafaili ya Dodoma Jiji

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la ufundi Yanga likiongozwa na kocha mkuu, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze wapo jukwaani wakifuatilia mchezo wa KMC dhidi ya Dodoma Jiji unaoendelea katika uwanja wa Uhuru.

Nabi ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika uwanjani hapa na kipindi cha pili Kaze aliwasili na kujiunga na mkuu wake.

Kaze alipofika alisalimiana na kocha mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm kisha alienda kukaa na Nabi kwenye jukwaa lingine.

Kitendo cha makocha hao kuwa jukwaani ni wazi wanaisoma Dodoma Jiji ambayo watacheza nayo baada ya mchezo wa Singida BS.

Yanga Alhamisi hii Novemba 16 itashuka dimbani dhidi ya Singida BsĀ  kisha watasafiri kwenda kucheza na Dodoma Jiji Novemba 22 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Katika mchezo huo, Dodoma Jiji imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya KMC. Mabao yote mawili ya Dodoma Jiji yamefungwa na Seif Kerihe, wakati bao la KMC likifungwa na Wazir Jr.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live