Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Jumapili ni Fainali kwetu

NABI CAF CC Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna kukwepesha jicho. Ndivyo unavyoweza kusema wakati Yanga wakijiandaa kuwavaa US Monastir siku ya Jumapili mchezo wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wamepania kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi katika mchezo huo, na katika kufanikisha hilo Kocha Mkuu wa Kikosi hicho anasema;

“Hii ni mechi ya fainali kwetu, tunakwenda kucheza mechi ngumu nyingine ya kundi letu, jambo zuri ni kwamba wachezaji wanajua kuwa wana deni la kujisahihisha kufuatia makosa ya mchezo wa kwanza wakijua sasa watacheza nyumbani mbele ya mashabiki wao ambao wamekuwa na heshima kubwa ya kuwafuata kokote wanakokwenda.” amesema Nasreddine Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live