Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi Bingwa wa Morocco, Wydad hatoshiriki CAFCL msimu ujao

Kocha Nabi Msz Nabi anachukua Ubingwa wa Morocco, Wydad chali

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya timu ya AS FAR Rabat kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya OC Safi katika muendelezo wa ligi kuu nchini Morocco ni rasmi sasa Wydad Casablanca wameondolewa katika mbio za ubingwa nchini humo.

AS FAR Rabat imefikisha alama 58 huku Wydad Casablanca wakiwa na alama 34 huku zikiwa zimebaki mechi 7 ambazo hata kama watashinda mechi zote hizo watafikisha alama 57 ambazo tayari AS FAR Rabat wameshazivuka.

Nafasi ya pili ni Raja Casablanca mwenye alama 54, tatu ni FUS Rabat alama 38 na wa nne ni RS Berkane mwenye alama 37.

Kwa mwenendo huu wa jeshi la Nabi katika ligi kuu nchini Morocco ni wazi kuwa Nabi anakwenda kuchukua ubingwa wa nchi hiyo na hivyo kutengeneza picha na taswira tofauti katika ubingwa wa nchi hiyo ambao umeshuhudiwa ukitawaliwa zaidi na timu Wydad na Raja.

Kwa takwimu hizo ni wazi kuwa, FAR Rabat na Raja Casablanca ndiyo timu pekee za Morocco zitakazocheza michuano Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu ujao ambapo Wydad ambaye atamaliza nje ya top 2, hatakuwa sehemu ya michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live