Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Aziz KI amefikia asilimia 50

Aziz Ki Pic 50 Kiungo Stephen Aziz Ki

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Yanga juzi usiku kilikuwa uwanjani kumalizana na Rhino Rangers ya Tabora katika mechi ya mwisho ya 32 Bora ya Kombe la ASFC, huku mabosi wa klabu hiyo walikuwa bado wanapambana na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyeikacha akishinikiza kuondoka mazima.

Lakini hali ikiwa hivyo, kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi amerudi nyuma kuanza kutengeneza upya silaha kama hiyo akiwaweka kikaangoni mastaa wake wawili ili kuhakikisha pengo la Fei Toto lisionekane kikosini wakati wakiendelea kwa mechi za mwisho wa msimu na zile za CAF.

Akiwa mazoezini, kocha Nabi ameanza kuwapika upya viungo wake wawili Stephane Aziz KI au ingizo jipya Mudathir Yahya kuwa na makali kama ya Fei Toto, aliyejiungia kikosi akiwa na mabao sita na asisti mbili akiiacha timu hiyo ikiongoza ligi ikisaka taji la msimu wa pili mfululizo.

Anachofanya Nabi amegundua kwamba licha ya ufundi wa Aziz KI ambaye ni fundi wa kutumia mguu wa kushoto, lakini bado hana ubora wa kusaidia kukaba timu yake inapopoteza mpira, kazi ambayo Fei toto alikuwa akiifanya ndani ya kikosi hicho.

Kugundua hilo Nabi amemkabidhi Aziz KI kwa mtaalam Helmy Gueldich kumpa mazoezi makali zaidi raia huyo wa Burkina Faso huku uwanjani akipewa uangalizi maalum wa kutakiwa kusaidia kukaba haraka timu inapopoteza mpira.

Nabi ameuwa mkali akiwa hataki kumuona Aziz KI akitembea na kumtaka kila wakati kuanza kutafuta mipira kwa kukaba huku kiungo huyo akipambana kwenda sawa katika hilo.

Akizungumzia hilo Nabi alisema bado Aziz KI hajafikiwa kiwango anachokitaka katika ubora wake wa kupambana uwanjani ambapo kwasasa yuko sawa na asilimia 50 tu ya vile anavyotaka.

“Tunajua hatupo na Feisal kwa sasa lakini lazima tuishi, ndio maana tunakazana na Aziz KI ambaye bado hajafika kile kiwango tunachotaka katika kusaidia kusaka mpira tunapoupoteza,” alisema Nabi na kuongeza;

“Kuna mazoezi maalumu ambayo tunampa kambini kuhakikisha anapandisha kiwango chake, katika mechi ambazo tunakwenda kucheza hatutakiwi kuwa na watu ambao watakuwa wanaangalia wapinzani wetu wakikimbilia langoni kwetu bila kupokonywa mpira.”

Upande wa pili kazi nyingine inafanyika pia kwa Mudathir ambaye hana shida katika ukabaji lakini akitakiwa kuwa na madhara makubwa zaidi kwa pasi zake na hata maamuzi ya kujaribu kwa mashuti akikaribia lango la wapinzani.

Hata hivyo, Mudathir anaonekana kuanza kwenda sawa na maagizo hayo akiwa na ubora wa kupiga mashuti yaliyonyooka kitu ambacho makocha wa Yanga wameendelea kumtengeneza zaidi.

“Tunahitaji Mudathir awe na madhara zaidi, sina shida naye katika kukaba, lakini nataka awe na ubora wa kukimbia haraka lango la wapinzani au kama atapiga pasi ndefu basi na yeye awe anasogea juu kwa haraka.

“Mechi za CAF ambazo tunakwenda kucheza tutakutana na viungo wenye kasi sana ambao tutatakiwa kuhakikisha hawatekelezi vyema majukumu yao kwa kutowapa nafasi hiyo.”

Chanzo: Mwanaspoti